
Msemaji wa Tume ya Uchaguzi Nawar Najmeh amesema matokeo ya awali yameanza kutolewa katika wilaya kadhaa baada ya wajumbe wa bodi za uchaguzi nao kupiga kura. Afisa huyo ameongeza kuwa majina ya washindi yatangazwa baadaye wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Uchaguzi huu ambao ni wa kwanza nchini Syria tangu kuangushwa kwa utawala wa rais Bashar al-Assad mnamo mwezi Desemba mwaka jana, umeibua pia wasiwasi kuhusu ujumuishaji hasa ikizingatiwa kuwa majimbo matatu hayakushiriki kutokana na sababu za kiusalama.