Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo, Oktoba 26, 2025, amewasili nchini Seychelles kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika hafla ya uapisho wa Rais mteule wa sita wa nchi hiyo, Dkt. Patrick Herminie.
Tume ya Uchaguzi ya Taifa ya Seychelles ilimtangaza Dkt. Herminie wa Chama cha United Seychelles (US) kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu, baada ya kumbwaga Rais aliyemaliza muda wake, Wavel Ramkalawan wa Chama cha Linyon Demokratik Seselwa (LDS).
Katika matokeo hayo, Dkt. Herminie alipata asilimia 52.7 ya kura, huku Rais Ramkalawan akipata 47.3%.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates