Chanzo cha picha, Getty Images
Aston Villa wamejiunga na Manchester United kutaka kumsajili mshambuliaji wa Brazil mwenye umri wa miaka 19 Endrick kwa mkopo kutoka Real Madrid mwezi Januari. (Daily Star on Sunday)
Hata hivyo, Lyon wanapewa nafasi kubwa ya kumpata Endrick, ambaye ana nia ya kuhama ili kushiriki katika mechi zaidi katika kikosi cha kwanza na kuboresha nafasi yake ya kujumuishwa katika kikosi cha Brazil kitakachoshiriki Kombe la Dunia la 2026. (Foot Mercato – In French)
Manchester United pia wanatazamiwa kuongeza juhudi zao za kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Elliot Anderson, 22, kutoka Nottingham Forest mwezi Januari, lakini wanaweza kukabiliana na ushindani kutoka kwa Chelsea, Manchester City na Newcastle United. (Offside)
Chanzo cha picha, Getty Images
Napoli wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United na England Kobbie Mainoo, 20, kwa mkopo mwezi Januari, kwa nia ya kufanya uhamisho huo kuwa wa kudumu msimu wa joto. (Mirror),
Wawakilishi wa mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford tayari wamefanya mazungumzo na Barcelona kuhusu masharti ya kandarasi, iwapo klabu hiyo ya Uhispania itabadilisha msimu mzima wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoka Manchester United kuwa uhamisho wa kudumu. (Sport – In Spanish), nje
Jukumu la Aston Villa kubadilisha uhamisho wa mkopo wa kiungo wa kati wa England Harvey Elliott kutoka Liverpool hadi uhamisho wa kudumu unafikiriwa kuanza iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 atacheza mechi 10 katika klabu hiyo ya Midlands. (Independent)
Chanzo cha picha, Getty Images
Paris FC wanataka kumnunua kiungo wa kati wa Ufaransa N’Golo Kante, 34, ambaye mkataba wake na Al-Ittihad unamalizika msimu ujao. (Foot Mercato – In Spanish In French)
Mshambulizi wa Mexico Santiago Gimenez, 24, ana hadi dirisha la uhamisho la Januari kuwashawishi AC Milan kwamba anastahili kusalia katika klabu hiyo badala ya kuuzwa. (Gazzetta dello Sport – In Italy)
Fowadi wa Italia Lorenzo Insigne, 34, ni mchezaji huru baada ya kuondoka Toronto FC na kushikilia kuhamia Lazio. (Soka Italia)