#HABARI: Watu wasiojulikana wamemshambulia kwa panga aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Bw#HABARI: Watu wasiojulikana wamemshambulia kwa panga aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Bw

#HABARI: Watu wasiojulikana wamemshambulia kwa panga aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Bw. Yusto Mapande, wakati akiingia nyumbani kwake, ambapo katika tukio hilo, Mapande alijeruhiwa mkononi na mguuni wakati akijitetea dhidi ya washambuliaji hao.

Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kulaani vikali kitendo hicho, akieleza kuwa tayari Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi ili kuwapata wahusika na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi wa Wilaya ya Same kuendelea kuchukua tahadhari wanapokuwa katika shughuli zao za kila siku, kuepuka unywaji wa pombe kupita kiasi, na kuhakikisha wanarejea nyumbani mapema endapo hakuna ulazima wa kuchelewa.

Kwa upande wake, Bw. Yusto Mapande, akizungumza baada ya kutembelewa na Mkuu wa Wilaya nyumbani kwake kwa ajili ya kumjulia hali, ameeleza kuwa watu waliomvamia walimfuata kwa kutumia pikipiki wakati akikaribia nyumbani huku akidhani ni wageni wenye nia njema.

Mapande amesema baada ya kushambuliwa alianza kuvuja damu nyingi na mwili wake kuanza kutetemeka, lakini kwa juhudi kubwa za madaktari wa hospitali ya Mji Same, aliweza kuokolewa na anaendelea vizuri.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *