
Maandamano makubwa yamefanyika nchini Israel leo Jumanne, Agosti 26. Waandamanaji wengi wameandamana katika maeneo mbalimbali nchini Israel wakipinga vita huko Gaza na kudai makubaliano ya kuachiliwa kwa mateka ambao bado wanashikiliwa katika Ukanda wa Gaza.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hii ni siku ya pili ya maandamano nchii Israel katika muda wa siku kumi kupinga mpango wa serikali wa kuanzisha mashambulizi katika maeneo ya mwisho ya eneo hilo la Palestina ambalo bado hayajadhibitiwa na jeshi la Israel. Serikali kwa upande wake imefanya kikao cha baraza la usalama kujadili hatua zinazofuata katika operesheni hizo. Operesheni hizi zinazua mjadala hata ndani ya makao makuu ya jeshi la Israel.
Eyal Zamir, mkuu wa jeshi la Israel mwenyewe, hajaficha upinzani wake dhidi ya mpango wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu. “Utamaduni wa kutoelewana ni sehemu isiyoweza kutenganishwa ya historia ya watu wa Israel,” alitangaza wakati wa mkutano na maafisa wakuu mapema mwezi huu. Kisha akaongeza: “Tutaendelea kueleza msimamo wetu bila woga.”
Hitilafu ya kimkakati
Eyal Zamir kisha alibainisha kwamba alichukulia mpango wa kuliteka Jiji la Gaza kama kosa la kimkakati. Kulingana naye, mpango huo unaweza kuhatarisha maisha ya mateka 20 wa Israel ambao bado wanazuiliwa huko Gaza na wale wa wanajeshi ambao wangejikuta wakishiriki katika operesheni ndefu na hatari. Hata hivyo, mara tu mpango huo ulipopitishwa, Eyal Zamir alitoa maagizo ya kuwakusanya askari wa akiba na kuanza kuwahamisha raia wa Gaza waliokuwa wakiishi katika maeneo husika.
Kulingana na Yediot Aharonot, tofauti hiyo inatokana na ratiba. Mkuu wa majeshi anaamini itakuwa vyema kufikia makubaliano ya sehemu na Hamas kwa ajili ya kuachiliwa kwa mateka. Majenerali wengine, hata hivyo, wako sambamba zaidi na serikali: ni makubaliano ya kina tu—kujisalimisha kwa Hamas—yanayoweza kuzuia kutekwa kwa Gaza. Na wao, kama Benjamin Netanyahu, wanashikilia ratiba ngumu, wakihofia kwamba mshirika wao Marekani hatimaye atataka kusitishwa kwa mapigano.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani, baraza la mawaziri la Israel, ambalo ajenda zake hazijawasilishwa rasmi, pia linatarajiwa kujadili kuanzishwa tena kwa mazungumzo kufuatia pendekezo la wapatanishi, Qatar, Misri na Marekani, ambalo lilikubaliwa na Hamas. Qatar, kwa upande wake, ilibainisha kuwa bado “inasubiri” jibu la Israel kwa pendekezo la hivi karibuni la wapatanishi wa usuluhishi unaoambatana na kuachiliwa kwa mateka, huku ikionyesha imani ndogo kwamba “ikiwa kungekuwa na ahadi, itakuwa nzuri.”