#HABARI: Nishati ni Uchumi vievile nishati ni mwanga, Mataifa makubwa yaliyofanikiwa kiuchumi ni yale yaliyofanikiwa kujitoshele…#HABARI: Nishati ni Uchumi vievile nishati ni mwanga, Mataifa makubwa yaliyofanikiwa kiuchumi ni yale yaliyofanikiwa kujitoshele…

#HABARI: Nishati ni Uchumi vievile nishati ni mwanga, Mataifa makubwa yaliyofanikiwa kiuchumi ni yale yaliyofanikiwa kujitosheleza katika uzalishaji wa nishati.

Takwimu zinabainisha kuwa katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru nchi yetu ilikuwa inazalisha MW za umeme 1,601.84 hadi mwaka 2021, hata hivyo Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa miaka minne katika kuendeleza na kuboresha mazuri ya watangulizi wake ameongeza uzalishaji wa umeme hadi MW
4,031.71 mwaka 2025, ndani ya kipindi kifupi vijiji vyote nchi hii vimefikiwa na huduma ya nishati ya umeme na asilimia 52 ya vitongoji vikiwa
vimefikiwa na huduma ya umeme.

Hakuna shaka kuwa ahadi hii itatimizwa ndani ya kipindi kifupi kijacho.

Mbali na nishati ya umeme, Rais Samia kwa kujali afya ya Watanzania hasa wanawake, alianzisha mkakati wa Nishati safi (2024-2034) wenye lengo la kuhakikisha matumizi ya nishati safi yanafikia asilimia 80.

Aidha, kwa mwaka 2024 serikali yake iligawa bure jumla ya mitungi ya gesi 452,445 kwa kaya 205,000.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
3m

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *