#HABARI: Baadhi ya wanachama wa Chama cha ACT-Wazalendo katika Jimbo la Mbulu-Vijijini, Wilaya ya Mbulu, Mkoani Manyara, wamepel…#HABARI: Baadhi ya wanachama wa Chama cha ACT-Wazalendo katika Jimbo la Mbulu-Vijijini, Wilaya ya Mbulu, Mkoani Manyara, wamepel…

#HABARI: Baadhi ya wanachama wa Chama cha ACT-Wazalendo katika Jimbo la Mbulu-Vijijini, Wilaya ya Mbulu, Mkoani Manyara, wamepeleka pingamizi la kumpinga Mgombea wa kiti cha ubunge kwa tiketi ya chama hicho Flatei Gregory kwenye ofisi ya msimamuzi wa uchaguzi jimbo la Mbulu vijijini kwa madai ya kuwa mgombea huyo hajafuata utaratibu halali wa chama hicho.

Wakitoa hoja zao wanachama hao wamesema hawajaridhishwa na utaratibu wa chama chao kumpokea na hatimaye kumpitisha kuwa mgombea wa Jimbo la Mbulu Vijijini bila kufuata utaratibu wa kikatiba.

Msimamizi wa uchaguzi katika Jimbo hilo Joseph Elia amesema amepokea mapingamizi hayo yaliyofikishwa ofisini hapo na kwamba amewaelekeza mapingamizi hayo yapelekwe ndani ya chama chao.

Ikumbukwe Flatei Gregory alikuwa Mbunge wa Mbulu vijijini kupitia CCM alijizolea umaarufu baada ya kupiga sarakasi bungeni na baada ya jina lake kutorudi akatimkia ACT na kuchukua fomu ya ubunge.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *