#HABARI: Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Lindi imemhukumu Salumu Moshi Mkumbwa (20), mkulima wa Mtanda, Manispaa ya Lindi, kifu…#HABARI: Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Lindi imemhukumu Salumu Moshi Mkumbwa (20), mkulima wa Mtanda, Manispaa ya Lindi, kifu…

#HABARI: Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Lindi imemhukumu Salumu Moshi Mkumbwa (20), mkulima wa Mtanda, Manispaa ya Lindi, kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka mwanafunzi wa miaka 16 wa kidato cha pili na kumsababishia maambukizi pamoja na maumivu makali.

Imeelezwa Mahakamani kuwa kwa nyakati tofauti kuanzia Desemba 2024 hadi Mei 13, 2025, majira ya saa 01:00 usiku, Salumu Moshi Mkumbwa alikuwa anamlaghai mwanafunzi huyo na kufanya naye mapenzi mpaka pale mama mzazi alipogundua baada ya kumfuatilia kisirisiri kwa muda na kisha kumfikisha mwanafunzi huyo Polisi kwa msaada zaidi. Jeshi la Polisi lilifanya upelelezi wa kina na kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Mtuhumiwa alifikishwa Mahakamani kwa ajili ya mashitaka yaliyokuwa yanamkabili, lakini alikana tuhuma hizo. Upande wa Jamhuri ulikuwa na vielelezo vinne na mashahidi watano waliotoa ushahidi wao, ambao ulimtia hatiani mtuhumiwa na Mahakama kutoa hukumu ya kwenda jela kifungo cha miaka 30.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *