#HABARI: Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Rais Dkt#HABARI: Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Rais Dkt

#HABARI: Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali imejipanga kushughulikia changamoto ya maji katika Mkoa wa Morogoro kwa kutekeleza miradi mipya na kulinda vyanzo vya maji.

Ameeleza haya atika mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Ngerengere, Morogoro Vijijini, ambapo Dkt. Samia amesema serikali imetekeleza miradi 15 ya maji tangu mwaka 2020, hatua iliyoongeza upatikanaji wa huduma hiyo kutoka asilimia 51 hadi asilimia 57.

Rais Samia ameongeza kuwa eneo la maji limepewa kipaumbele maalum katika mpango wa serikali yake kwa miaka mitano ijayo, likiwemo kuhakikisha miradi ya umwagiliaji inafanikiwa na huduma ya maji inawafikia wananchi wengi zaidi.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *