#HABARI: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt#HABARI: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt

#HABARI: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuendelea kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta za afya na elimu mkoani Morogoro.

Akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Viwanja vya Tumbaku, Mjini Morogoro, jioni ya Agosti 29, 2025, Dkt. Samia amesema Serikali ya CCM imepanga kujenga vituo vya afya 28 na zahanati 67 katika wilaya mbalimbali za mkoa huo.

Amebainisha pia kuwa Serikali itakamilisha ujenzi wa miundombinu ya maabara, jengo la upasuaji na kituo cha afya katika eneo la Tungi, pamoja na ujenzi wa wodi ya mama na mtoto katika Kituo cha Afya Mafiga.

Aidha, amesisitiza kuwa Serikali itaendeleza uwekezaji katika sekta ya elimu kwa kujenga madarasa 190 ya shule za sekondari na shule mpya ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Ameongeza kuwa sera ya elimu bila ada itaendelea kutekelezwa ili kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanafikiwa na elimu.

Dkt. Samia yuko mkoani Morogoro kuendelea na mikutano ya kampeni za CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *