#HABARI: Viongozi wa Kimila wa makabila takribani 18 mkoani Morogoro, na Wazee wa kimila wamefanya Tambiko maalum, lenye lengo la kumpatia baraka na kumkaribisha Mgombea wa Urais, kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt.Samia Suluhu Hassan na kumuwezesha kufanikisha kampeni za kunadi Sera za Chama hicho.
Viongozi hao wa Kimila maarufu kama Machifu, wamefanya Tambiko hilo eneo maalum la Kihistoria mkoani humo.
Naye Mkuu wa mkoa wa morogoro Bw. Adam Malima, ameeleza umuhimu wa kushirikisha Wazee hao katika mambo yanayoendelea ndani na nje ya Mkoa.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania