Shirika la mpango wa Chakula duniani,WFP, limeanza kutekeleza mpango wa kupunguza chakula cha msaada hadi asilimia 60 Aidha WFP imewaweka wakimbizi kwenye makundi mapya ,tofuati na awali ambapo wale wenye uhitaji mkubwa wa msaada wakiwa wanawake ,watoto na walemavu  wanapewa kipau mbele ,hii pia ikiwa chanzo cha maandamano ya kila mara katika kambi za wakimbizi ikiwemo kambi ya Kakuma ,eneo la Turkana kaskazini mwa Kenya.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya punguzo  ikiwalazimisha wakimbizi  kutoka nje ya kambi kutafuta njia mbadala kujikimu kimaisha baada ya  wengi kubaki  bila msaada wanaohitaji.

Katika kambi ya Kakuma kaskazini mwa Kenya,wakimbizi  wanabidi kufanya kazi ambazo zinawapa malipo duni ya hadi shilingi mia moja.

Shirika la mpango wa chakula duniani,WFP limepunguza mgao wa chakula kwa wakimbizi
Shirika la mpango wa chakula duniani,WFP limepunguza mgao wa chakula kwa wakimbizi © ICRC

Wanaofanya kilimo pia kilio chao ni kuwa wanunuzi ambao ni wengi hawana pesa kununua bidhaa zao.

Waliofungua biashara katika kambi wanabidi kukaa na bidhaa kwa muda mrefu bila kununuliwa wengine wakikopa bila kulipa madeni yao.

Nje ya kambi ,wafanyabiashara pia wanasema wateja wao wengi ambao ni mashirika ya kimsaada au wafanyakazi katika mashirika hayo ,hawana pesa hivyo hawawezi kufanya manunuzi au kulipia huduma za kawaida kama awali.

Kakuma Motors ni miongoni mwa kampuni zinazokadiria hasara kutokana na punguzo la msaada kwa wakimbizi
Kakuma Motors ni miongoni mwa kampuni zinazokadiria hasara kutokana na punguzo la msaada kwa wakimbizi © Carol Korir

Kambi ya Kakuma ina wakimbizi zaidi ya laki tatu kutoka Sudan,Sudan Kusini,Somalia,Burundi,Ethiopia na hata Eritrea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *