Nchini Sudan, takriban watu 19 wameuawa katika mashambulizi ya anga huko Darfur. Shambulio lililohusishwa na jeshi la Sudan kwenye kliniki ya Nyala, Darfur Kusini, lilisababisha vifo vya watu kumi na wawili siku ya Jumamosi, Agosti 30. Sambulio hilo lililohusishwa na wanajeshi siku ya Jumamosi jioni katika mji wa al-Fasher pia lilisababisha vifo vya watu tisa. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa zaidi ya mwaka mmoja, mji mkuu wa Darfur Kaskazini umekuwa ukizingirwa na wanamgambo wanaojaribu kuchukua udhibiti wa mji huo kutoka kwa jeshi la Sudan. Kulingana na waangalizi, mashambulizi yameongezeka kwa kasi katika mji huo katika muda wa wiki mbili zilizopita.

Katika mji wa al-Fasher, milipuko ya mabomu hutokea kila siku, mkaazi mmoja amesema. Siku kadhaa, wanamgambo hushambulia hadi mara tatu kwa siku kwa risasi na mabomu, wakati mwingine kwa ndege zisizo na rubani. Kwa mujibu wa waangalizi wa mambo, Vikosi vya Msaada wa Haraka vya Jenerali Hemedti vimeongeza mashambulizi maradufu katika siku za hivi karibuni, hasa magharibi mwa mji huo, katika jaribio la kuudhibiti uwanja wa ndege ambao bado uko mikononi mwa jeshi la Sudan.

Kwa wakazi, maisha yamekuwa magumu, anasema Mohamed Doda. “Kila kitu kimekuwa hatari sana. Kuchota maji au chakula imekuwa hatari. Wakati mashambulizi yanapoanza, kila mtu anajificha kwenye mashimo yaliyochimbwa ardhini au kwenye makontena yaliyozikwa ardhini, ambayo hutumika kama makazi. Kwa bahati mbaya, RSF inalenga makazi haya. Wanajaribu kuwalazimisha watu kukimbia ili kuchukua udhibiti wa jiji,” anafafanua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *