
Watu wasiopungua 14 wameuawa Jumanne jioni, Septemba 2, wakati mshambuliaji wa kujitoa mhanga alipojilipua katika mkutano wa kisiasa huko Balochistan, maafisa wawili kutoka mkoa wenye machafuko kusini magharibi mwa Pakistan wameliambia shirika la habari la AFP.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Maafisa hao wa serikali ya mkoa ambao hawakutaka kutajwa majina yao kwa kuwa hawakuruhusiwa kuzungumza na waandishi wa habari, wameongeza kuwa watu 18 wamejeruhiwa katika mlipuko huo uliotokea katika eneo la kuegesha magari la uwanja ambapo mamia ya wanachama wa chama cha Balochistan National Party (BNP) walikuwa wamekusanyika.
Maafisa hao wameongeza kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga huko Quetta.
Mlipuaji wa kujitoa mhanga, wamesema, alifyatua mkanda uliokuwa umejaa vilipuzi katika eneo la kuegesha magari ambapo mamia ya wanachama wa Balochistan National Party (BNP) walikuwa wamekusanyika.
Kiongozi wake, Akhtar Mengal, ambaye alikuwa akitoka kwenye mkutano huo baada ya kutoa hotuba wakati wa shambulio hilo, amesema kenye mtandao wa kijmii wa X kwamba yuko “salama salimini” lakini “ameumizwa na kupoteza wafuasi.”
Katika hatua hii, hakuna aliyedai kuhusika na shambulio hilo.
BNP inadai kuwa mtetezi wa walio wachache wa Baloch, ambao wanasema wamenyimwa fursa katika jimbo hili linalopakana na Iran na Afghanistan, lenye utajiri wa madini na hidrokaboni, bado maskini zaidi nchini Pakistan.
Huko Balochistan, rasmi, asilimia 70 ya wakazi ni maskini, ingawa ardi ina akiba kubwa zaidi ya madini ambayo hayajatumika duniani, na miradi mikubwa, hasa kutoka China, inazalisha mapato makubwa.
“Saa kumi na mbili” za urushianaji risasi
Uasi wenye silaha unastawi katika ardhi hii yenye rutuba, na Balochistan ilishuhudia ongezeko kubwa zaidi la ghasia nchini Pakistan mwaka wa 2024: ongezeko la 90%, kulingana na Kituo cha Utafiti na Mafunzo ya Usalama huko Islamabad, na vifo 782.
Kundi la watu waliojitenga kilifanya utekaji nyara wa kutisha kwenye treni hapo mwezi Machi.
Tangu Januari 1, kulingana na hesabu ya AFP, zaidi ya watu 430, wengi wao wakiwa wanachama wa vikosi vya usalama, wameuawa katika ghasia zilizotekelezwa na kundi yenye silaha yanayopigana na jimbo hilo, huko Balochistan na mkoa jirani wa Khyber-Pakhtunkhwa.
Siku ya Jumanne, huko Balochistan, wanamgambo watano waliuawa na wanne kujeruhiwa wakati bomu lililotegwa kando ya barabara lilipolipuka wakati msafara wao ukipitia wilaya karibu na mpaka wa Iran, afisa mkuu wa eneo hilo ameiambia AFP.
Kwa kuongezea, wanajeshi sita waliuawa katika shambulio kwenye makao makuu ya wanajeshi huko Khyber-Pakhtunkhwa, jeshi limeripoti. Watu kumi na saba, wakiwemo raia, walijeruhiwa, afisa mmoja wa eneo hilo ameongeza, katika shambulio hili lililodaiwa na kundi dogo lenye uhusiano na kundi la Taliban la Pakistan.
Majibizano ya risasi kati ya vikosi vya usalama na watu wenye silaha ambao walianzisha shambulio kwenye kambi hiyo kwa “gari ikigonga na kisha washambuliaji watano wa kujitoa mhanga,” kulingana na afisa huyu wa serikali ya eneo hilo, ilichukua “saa kumi na mbili” kabla ya “magaidi sita kuuawa.”
Mwaka wa 2024 ulikuwa mbaya zaidi katika karibu muongo mmoja nchini Pakistan, na vifo zaidi ya 1,600, karibu nusu yao ni askari na maafisa wa polisi, kulingana na Kituo cha Utafiti na Mafunzo ya Usalama chenye makao yake mjini Islamabad.