Maelfu ya askari wa akiba wameanza kuripoti kazini huku jeshi la Israel likiendelea na mashambulizi ya kuiteka Gaza. Mji huo pia uko chini ya mashambulizi makali ya anga na mizinga ya Israel, na hospitali za eneo hilo zinaripoti kuwa zaidi ya Wapalestina 50 wameuawa katika mji huo tangu usiku wa manane.
