Baada ya Los Angeles na Washington, Donald Trump analenga ngome nyingine ya chama cha Democratic: Chicago, mji mkuu wa Illinois. “Tutaingilia kati” katika mji huo, Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza siku ya Jumanne, Septemba 2, bila kutaja ni lini amepanga kupeleka vikosi vya usalama vya shirikisho katika mji huo, kama ilivyokuwa katika mji mkuu wa Marekani tangu katikati ya mwezi Agosti.
