Kufuatia kushuka kwa kasi kwa misaada ya maendeleo ya Marekani, kupungua kwa misaada kwa shughuli za kulinda amani kunatia wasiwasi Umoja wa Mataifa. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita, Donald Trump alifuta msaada wa dola bilioni 4.9 wa msaada wa kigeni ambao ulikuwa umeidhinishwa na Baraza la Congress. Kati ya msaada huu, dola milioni 800 zilikuwa za kufadhili shughuli za ulinzi wa amani duniani kote, nusu yake zikitengwa kwa bara la Afrika. Kulingana na Umoja wa Mataifa, hii inaweza kuhatarisha usalama wa raia, haswa nchini Sudan Kusini na DRC.

Nchini Marekani, utawala wa Trump umekosoa vikali operesheni za kulinda amani. Katika risala yake kwa Baraza la Congress, utawala wa Trump unashtumu kushindwa kwa misheni nchini Mali, DRC, na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Umetaja mabilioni ya dola zilizotumika, ukashutumu miradi mikubwa ya ufisadi, na kutaja ubadhirifu. Pia umetaja visa vya uchimbaji madini na unyanyasaji wa kingono nchini DRC na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Donald Trump pia anashutumu Umoja wa Mataifa kwa kutumia pesa zilizotengwa kudumisha usalama kwa madhumuni mengine. Umoja wa Mataifa unakabiliwa na mzozo mkubwa wa ukwasi, pungufu ya dola bilioni 2.7 kufadhili shughuli za kulinda amani.

Chini ya shinikizo, Umoja wa Mataifa umeandaa mpango wa kubana matumizi unaoitwa UN 80. Mpango huu unajumuisha kusimamisha uajiri, kubana matumizi, na kusimamishwa kwa baadhi ya shughuli. Kwa mujibu wa ripoti ya chombo cha habari cha Africa Intelligence, kuondolewa kwa wanajeshi 4,000 wa kulinda amani kutoka kwa ujumbe wa MONUSCO nchini DRC kunajadiliwa, sawa na karibu theluthi moja ya wanajeshi waliotumwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Marekani pia imekataa kufadhili, kupitia Umoja wa Mataifa, ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini Somalia, AUSSOM, ulioanzishwa kupambana na magaidi wa Al Shabab. Operesheni hii bado inatafuta mpango thabiti wa ufadhili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *