Ikulu ya Élysée itaandaa mkutano wa “muungano wa walio tayari” kwa ajili ya Ukraine leo Alhamisi, Septemba 4, huku Volodymyr Zelensky akihudhuria. Viongozi kadhaa wa Ulaya wanatarajiwa kusafiri kwenda Paris, wakati wengine watashiriki kwa njia ya video. Mkutano huu, ulioitishwa na Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, ulitanguliwa siku ya Jumatano, Septemba 3, na chakula cha jioni kati ya marais wa Ufaransa na Ukraine.
