Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesisitiza kuwa Uturuki haitakaa kimya wakati Wapalestina wakiteseka chini ya mashambulizi ya Israel, akimsuta Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

“Hatuwezi kukaa kimya kama watazamaji wa mateso huko Palestina au ukandamizaji wa dhalimu, yule kafiri anayeitwa Netanyahu,” Erdogan alisema Jumatano, akihutubia tukio la ufunguzi wa Wiki ya ‘Mevlid-i Nebi’ ambayo ni hafla ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW), iliofanyika jijini Ankara.

Rais aliongeza kuwa wasiwasi wa Uturuki unaenea nje ya mipaka yake, akisisitiza mshikamano na mataifa ya Kiislamu yaliyokumbwa na migogoro.

“Nusu ya mioyo yetu iko hapa; nusu nyingine iko Gaza, Palestina, Yemen, Sudan na Afghanistan, ambapo majeraha ya ulimwengu wa Kiislamu yanavuja damu,” alisema.

Akisisitiza mada ya umoja, Erdogan alisema: “Tunaona Waislamu wote kama matofali ya jengo moja, na viungo vya mwili mmoja.”

Licha ya machafuko katika eneo lote, rais alihimiza kuwe na uvumilivu na ukaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *