
Miili zaidi ya 370 imepatikana baada ya maporomoko mabaya ya ardhi yalisababisha vifo vya karibu watu 1,000 Darfur magharibi mwa Sudan, kundi moja la Sudan lilisema siku ya Alhamisi.
Ibrahim Hasbullah, afisa wa Sudan Liberation Movement (SLM), anasema wamefanikiwa kupata miili zaidi ya 370 kutoka kwenye kifusi katika kijiji cha Tarsin eneo la Kati la Jimbo la Darfur.
“Kwa wale wengine waliofariki, hatukuweza kutoa miili yao kwa kuwa ilikuwa iko chini ya miamba ilhali wengine walisombwa na mabonde,” aliongeza katika video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Katika taarifa siku ya Alhamisi, SLM ilisema kijiji hicho kilokumbwa na mkasa “kiko katikati ya Jebel Marra, mchanga wa volkano ambao hauwezi kuhimili maporomoko pindi kunapokuwa na mvua kubwa.”