Chanzo cha picha, Getty Images
Huko nyuma katika miaka ya 1980 wakati mtandao ulikuwa bado mchanga, nchi zilikuwa zikikabidhiwa anwani zao za kipekee za tovuti ili kuvinjari ulimwengu huu mpya wa mtandaoni. Kama vile .us kwa Marekani au .uk kwa Uingereza.
Hatimaye, karibu kila nchi na eneo lilikuwa na anuani yake kwa misingi ya jina lake la Kiingereza au lugha yake. Hii ilijumuisha kisiwa kidogo cha Carribean cha Anguilla, ambacho kilipata anwani .ai.
Bila kujua Anguilla wakati huo, hii ingekuwa bahatinasibu yake ya baadaye.
Kutokana na kuongezeka kwa kasi kwa Akili Mnemba (AI), makampuni na watu binafsi zaidi na zaidi wanalipa Anguilla, iliyo chini ya Uingereza, ili kusajili tovuti mpya kwa kitambulisho cha neno .ai.
Kama vile bosi wa teknolojia wa Marekani, Dharmesh Shah, ambaye mapema mwaka huu alitumia taarifa ya $700,000 (£519,000) kwenye anwani you.ai.
Akizungumza na BBC, Bw Shah anasema aliinunua kwasababu alikuwa na “wazo la bidhaa ya AI (akili Mnemba) ambayo ingeruhusu watu kuunda matoleo yao ya kidijitali ambayo yangeweza kufanya kazi maalum kwa niaba yao”.
Idadi ya tovuti za .ai imeongezeka zaidi ya mara 10 katika miaka mitano iliyopita, na imeongezeka maradufu katika kipindi cha miezi 12 pekee, kulingana na tovuti inayofuatilia usajili wa majina yake.
Changamoto kwa Anguilla, ambayo ina idadi ya watu 16,000 tu, ni jinsi ya kutumia bahati hii ya faida kubwa na kuigeuza kuwa chanzo cha mapato cha muda mrefu na endelevu.
Sawa na visiwa vingine vidogo vya Carribean, uchumi wa Anguilla umejengwa kwenye msingi wa utalii. Hivi majuzi, imekuwa ikiwavutia wageni katika soko la usafiri wa kifahari, hasa kutoka Marekani.
Idara ya takwimu ya Anguilla inasema kulikuwa na rekodi ya idadi ya wageni katika kisiwa hicho mwaka jana, huku watu 111,639 wakiingia katika ufuo wake.
Bado sekta ya utalii ya Anguilla iko katika hatari ya kuharibiwa na vimbunga kila msimu wa vuli. Ikiwa kaskazini-mashariki mwa safu ya kisiwa cha Carribean Anguilla iko kikamilifu ndani ya ukanda wa kimbunga wa Atlantiki ya Kaskazini.
Kwa hivyo kupata mapato yanayoongezeka kutokana na uuzaji wa anwani za tovuti ambazo zinachangia pakubwa katika kuleta uchumi wa kisiwa hicho. Hili ni jambo ambalo Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) lilibainisha katika ripoti ya hivi majuzi kuhusu Anguilla.
Chanzo cha picha, HubSport
Katika rasimu yake ya hati ya bajeti ya 2025, serikali ya Anguillian inasema kuwa mwaka wa 2024 ilipata dola milioni 105.5 za Carribean Mashariki ($39m; £29m) kutokana na kuuza majina ya anwani za mtandao. Hiyo ilikuwa karibu robo (23%) ya jumla ya mapato yake mwaka jana. Utalii unachangia baadhi ya 37%, kulingana na IMF.
Serikali ya Anguillian inatarajia mapato yake ya anwani yake ya .ai kuongezeka zaidi hadi dola 132m za Carribean Mashariki mwaka huu, na hadi 138m mwaka wa 2026. Inakuja kwani zaidi ya vikoa 850,000 .ai sasa vipo, kutoka chini ya 50,000 mwaka wa 2020.
Kama eneo la Uingereza la ng’ambo, Anguilla iko chini ya uhuru wa Uingereza, lakini kwa kiwango cha juu cha kujitawala kwa ndani.
Uingereza ina ushawishi mkubwa katika ulinzi na usalama wa kisiwa hicho, na imetoa usaidizi wa kifedha wakati wa shida. Baada ya Kimbunga Irma kuiharibu vibaya mnamo 2017, Uingereza ilitoa pauni milioni 60 kwa Anguilla kwa miaka mitano kusaidia kukidhi bili ya ukarabati.
Wizara ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Uingereza imeiambia BBC inakaribisha juhudi za Anguilla “kutafuta njia bunifu za kuleta ukuaji wa uchumi” kwani inasaidia “kuchangia kujitosheleza kifedha kwa Anguilla”.
Ili kudhibiti mapato ya jina la anwani yake kinachoendelea kukua, mnamo mwezi Oktoba 2024, Anguilla alisaini mkataba wa miaka mitano na kampuni ya kiteknolojia ya Marekani iitwayo Identity Digital, ambayo inajishughulisha na usajili wa majina ya anwani za mtandao.
Mwanzoni mwa mwaka huu, Identity Digital ilitangaza kuwa imehamia ambapo vikoa vyote vya .ai vimepangishwa, kutoka kwa seva za Anguilla, hadi mtandao wake wa kimataifa wa seva. Hii ni kuzuia usumbufu wowote kutoka kwa vimbunga vya siku zijazo, au hatari nyingine yoyote kwa miundombinu ya kisiwa hicho, kama vile kukatika kwa umeme.
Gharama halisi ya anwani za .ai haijafichuliwa hadharani, lakini bei za usajili zinasemekana kuanza kutoka takriban $150 hadi $200. Pamoja na ada za upya wa karibu kiasi sawa kila baada ya miaka miwili.
Wakati huo huo, kadri majina ya anwani yanavyohitajika zaidi ndivyo yanavyouzwa kwa mnada, huku baadhi yake yakipata mamia ya maelfu ya dola za Marekani. Wamiliki wa anwani hizi wanapaswa kulipa ada ndogo sawa za upya kama kila mtu mwingine.
Katika hali zote, serikali ya Anguilla inapata mapato ya mauzo, na Identity Digital ikipata mgao wake unaosemekana kuwa ni wa karibu 10%.