
Wanajihadi wanaoshirikiana na Al-Qaeda, wameendeleza mashambulio kulenga viwanda vinavyomilikiwa na wawekezaji wa kijeshi hasa, Wachina.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Umoja wa Mataifa, kwenye ripoti yake hivi karibuni kuwa, mbinu hii inatumiwa na uongozi wanajihadi hao kutishia uongozi wa kijeshi.
Aidha, lengo ni kutishia uongozi wa kijeshi na kuendelea kuwashinikiza wanajeshi kuondoka madarakani na kuanza kutekeleza uongozi wa sharia.
Mwezi Juni, kundi la JNIM, lilionya kuwa lilikuwa limewaandaa wapiganaji wake, kushambulia viwanda vyote vya kigeni, vinavyosimamiwa na wanajeshi baada ya kuchukua madaraka mwaka 2020 na 2021.
Wanajihadi hao mwezi Julai, walitekeleza vitisho vyake kwa kushambulia viwanda saba vya kigeni zinazojihusisha na uzalishaji wa dhahabu.
Uwekezaji wa viwanda vya China nchini Mali, umekuwa ukiongezeka katika miaka ya hivi karibuni, kati yam waka 2009 hadi 2024 wakati serikali ya China ilipowekeza kiasi cha Dola Bilioni 1.6 kuimarisha sekta ya viwanda.