Mamlaka ya afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wako katika hali ya tahadhari kufuatia kugunduliwa kwa mlipuko mpya wa virusi vya Ebola. Eneo lililoathiriwa ni mkoa wa Kasai, katikati mwa nchi. Tangu Agosti 20, karibu wagonjwa thelathini wamethibitishwa, na angalau vifo 16, wakiwemo wafanyakazi kadhaa wa afya.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tahadhari hiyo ilitolewa baada ya kulazwa kwa mama mjamzito katika eneo la afya la Bulape ambaye alionyesha dalili za ugonjwa wa Ebola. Kulingana na mamlaka ya afya, ugonjwa wa Ebola, ambao umegunduliwa huko Kasai, unasababishwa na kinachojulikana kama aina ya virusi vya Zaire, ambayo chanjo ipo. “Lakini ili kuisafirisha, tunahitaji kuhakikisha vifaa,” amebainisha Waziri wa Afya Samuel Kamba.

Hili ni mlipuko wa kumi na sita kuathiri nchi hii tangu ugonjwa huo kutambuliwa mnamo mwaka 1976. Na ni janga la tatu katika eneo hili la Kasai, linalopakana na Tshuapa, na Sankuru. Ni eneo gumu sana kufikiwa, lililotengwa, na lenye mfumo dhaifu wa afya.

Mamlaka inajiandaa kukabilina na ugonjwa huo, lakini mamlaka inatarajia idadi ya vifo kuongezeka na ugunduzi wa wagonjwa wapya ambao wanaweza kuwa wapo kabla ya mgonjwa wa kwanza kulazwa hospitalini, kwani sio lazima wagonjwa wote waende kwenye vituo vya afya. Waziri pia ametoa wito kwa raia kutoa taarifa ya mtu yeyote mwenye dalili za ugonjwa huo ili kupunguza hatari ya kuenea kwa ugonjwa huo hatari.

“Tunajua tu kuhusu mlipuko ikiwa tunajua kisa cha fahirisi”

Pamoja na mamlaka ya Kongo, Shirika la Afya Duniani, ambalo limetuma timu katika eneo hilo, na Afrika CDC, Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa vya Umoja wa Afrika, vinafanya kazi. Mkurugenzi wake Dkt Jean Kaseya amewasili mjini Kinshasa. Kwake, moja ya vipaumbele ni kupata asili ya janga hilo. “Hatuwezi kukabiliana na janga ambalo hatujui, na tunajua tu juu ya mlipuko ikiwa tunajua kesi ya fahirisi,” anafafanua. “Kwa sababu kwa visa vya fahirisi, tunajua miezi ya maambukizi, tunajua kiwango kwa vile tunajua jinsi ya kuweka ramani ya eneo vizuri, na pia tunajua jinsi maambukizi yalivyotokea. Na tunaweza pia kupata taarifa nyingine kwa kujua asili ya mlipuko huo.”

Kupata asili ni ufunguo wa kukomesha janga hili haraka iwezekanavyo, kwani chanjo ipo. “Tuna zaidi ya dozi 2,000 za chanjo,” anathibitisha. “Tuna ugavi mzuri wa antimonoclonals, ambazo ni dawa tulikuwa tukitumia. Tunahitaji tu kutumia vifaa ili kuzisafirisha.” Nimekuja DRC siku ya kwanza kwa sababu nimetaka kuhakikisha kwamba, pamoja na serikali, tunakomesha haraka mlipiko huo. Ni kwa maslahi yetu leo ​​kuhakikisha kwamba mlipuko huu sio tu unabakia, lakini pia lunaisha haraka sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *