
Ni mojawapo ya nchi zinazochangia kwa uchache katika ongezeko la joto duniani, lakini pia ni mojawapo ya nchi zilizo hatarini zaidi kwa madhara yake. Tangu mwezi Juni, eneo la kaskazini mashariki mwa Pakistani limekumbwa na mafuriko makubwa. Kulingana na ripoti ya hivi punde, watu 884 wamepoteza maisha na zaidi ya wakaazi milioni moja wamelazimika kuhamishwa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Geneva, Jérémie Lanche
Vijiji vyote viko katika maji, madaraja yamesombwa na maji, maelfu ya ng’ombe wamekufa maji, na watu walionusurika wamepoteza kila kitu kwa dakika chache… Picha kutoka Pakistan zinakumbusha zile za mwaka wa 2022, wakati hali sawa na hiyo iliposababisha vifo vya zaidi ya watu 1,700 na kulazimu Wapakistani milioni 8 kuhama makazi yao. “Bado hali hiyo haijafikia,” anasema Farid Abdulkadir Aiywar, mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu nchini Pakistan.
Ingawa idadi ya vifo ni kubwa, inaweza kuwa mbaya zaidi. “Mengi yalifanyika kuzuia maafa,” anasisitiza Farid Abdulkadir Aiywar. Mkoa wa Punjab, ambako wanaishi nusu ya watu milioni 250, ndio ulioathirika zaidi. “Unapoangalia kiasi kikubwa cha mvua iliyonyesha, sio kupuuzia kile kilichotokea – vifo 884 ni vingi – tungeweza kuwa na waathirika wengi zaidi,” anabainisha.
Jukumu kubwa la mabadiliko ya tabianchi
Mvua hizi kubwa huambatana na msimu wa monsuni, lakini mabadiliko ya tabianchi yanaongeza kasi yake, anaeleza Clare Nullis wa Shirika la Hali ya Hewa Ulimwenguni: “Kwa kila kiwango cha ziada cha ongezeko la joto, angahewa ina unyevu zaidi wa 7%. Hii ina maana kwamba mvua inaponyesha, inanyesha zaidi na kuna hatari kubwa ya mafuriko.”
Utabiri wa hali ya hewa sio wa kutia moyo. Mafuriko mapya yanaweza kutokea katika siku zijazo, ikiwa ni pamoja na katika mji mkuu, Islamabad.