Somalia: Al Shabab wanadai kutekeleza shambulio dhidi ya wanajeshi wa MarekaniSomalia: Al Shabab wanadai kutekeleza shambulio dhidi ya wanajeshi wa Marekani

Nchini Somalia, kundi la kigaidi la Al-Shabab lilitekeleza shambulizi siku ya Alhamisi dhidi ya kambi ya kijeshi karibu na uwanja wa ndege wa Kismayo, mji wenye bandari ulioko kusini mwa nchi hiyo. Kwa mujibu wa Kamandi ya Marekani barani Afrika (AFRICOM), ambayo ilitangaza tukio hilo, hakuna hasara yoyote iliyopatikana kwa upande wa wanajeshi. Shambulio hili linakuja mara tu baada ya ziara ya kamanda mpya wa AFRICOM mjini Mogadishu na, linafichua uwepo wa wanajeshi wa Marekani nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *