
Shambulio jipya kubwa limehusishwa na ADF/MTM mashariki mwa DRC usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne, Septemba 9. Mashirika ya kiraia yanaripoti kuwa watu wasiopunguwa 72 waliuawa na nyumba kumi na nne kuchomwa moto.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Shambulio hilo lilitokea Ntoyo, mashariki mwa Manguredjipa, katika eneo la Bapere katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Kwa mujibu wa Cyprien Sangala, mratibu wa shirika la kiraia la Renadel, “kilichotokea kwa hakika ni kitendo ambacho tunakielezea kuwa kisicho cha kibinadamu. Ni mauaji ya raia 72 waliouawa kwa njia za kinyama. Miongoni mwao ni wanawake, wanaume na watoto. Familia nzima iliangamizwa. Kulingana na shahidi, wapiganaji 40 waliokuwa na silaha nzito ndio walitekeleza ukatili huo.” Walizunguka mtaa mzima na kuanza kuvunja milango kwa nguvu. Ni nyumba chache tu na maduka yalikuwa bado yamefunguliwa, na walikuwa wamezungukwa na majambazi hawa. Washambuliaji hao pia walilenga mahali pa maombolezo ambapo makumi ya watu, wengi wao wakiwa wanafamilia, walikuwa wamekusanyika.
Siku ya Jumanne, pamoja na maombolezo hayo, wakazi pia walijawa na hasira na sintofahamu kutokana na kuendelea kwa mauaji hayo. Wanahisi kutelekezwa, licha ya kuwepo kwa operesheni ya pamoja kati ya majeshi ya Kongo na Uganda yanayodaiwa kuongoza mashambulizi dhidi ya kundi linaloshirikiana na Islamic State. Cyprien Sangala amekutana na wawakilishi wengine wa mashirika ya kiraia ya eneo hilo siku ya Jumanne. Waliamua kudai uwajibikaji na maelezo kutoka kwa mamlaka.
“Mashirika ya kiraia yanataka serikali kutoa maelezo juu ya mauaji ya mara ya kumi dhidi ya watu, ambao wanataka kuona kundi la ADF likisakwa rasmi na jeshi. Kulikuwa na tahadhari wiki moja kabla ya mauaji hayo, lakini hakuna aliyejibu,” analaumu.