Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), hali ya utulivu imerejea katika jiji la Uvira kufuatia maandamano ya siku ya Jumatatu, Septemba 8, ambayo yaligraimu maisha ya mtoto wa miaka 12 na kuwajeruhi wengine kumi. Maandamano haya yaliitishwa na sehemu ya mashirika ya kiraia na wanamgambo wa Wazalendo, ambao wanadai kuondoka kwa afisa wa jeshi, anayechukuliwa kuwa karibu sana na waasi wa AFC/M23. Ujumbe wa serikali unatarajiwa Uvira.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mji wa Uvira umekuwa chini ya mvutano kwa siku tisa. Maduka, biashara mbalimbali na shule bado zimefungwa. Wanamgambo wa Wazalendo, ambao sasa wanaungwa mkono na baadhi ya mashirika ya kiraia, wanamtaka Jenerali Olivier Gasita, naibu kamanda wa kanda ya 33 la kijeshi kuondoka katika mji huo. Anadaiwa kuwa karibu na AFC/M23 kwa sababu ya asili yake ya kuwa Munyamulenge, jamii ya Watutsi wachche wa Kongo.

Mwishoni mwa juma lililopita, uongozi wa juu mjini Kinshasa ulithibitisha tena kumuunga mkono, na kuongeza kuwa “askari hatumikii kabila anakotoka, anatumikia taifa zima.” Lakini hii haikutosha kutuliza hasira za wengine. Ujumbe wa serikali unatarajiwa mjini Uvira kutafuta suluhu, ametangaza Spika wa Bunge la taifa Vital Kamerhe.

Wito wa kuwasikiliza wabunge

Kwa upande wao, wabunge tisa wa mkoa wa Kivu Kusini wameitaka serikali kuwasikiliza wananchi, huku wakikumbusha kuwa maeneo ya Uvira na Fizi ndio kikwazo kikubwa kilichokwamisha kusonga mbele kwa waasi wa AFC/M23, kutokana na ushirikiano kati ya jeshi na Wazalendo. Wameitaka Kinshasa kuwaunga mkono wanamgambo hao wazalendo.

Kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi, ambacho hakikutoa maelezo zaidi, Jenerali Gasita ameondoka Uvira. Mtafiti aliyewasiliana na RFI amesema Wazalendo wameweka wosia wao huko Kivu Kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *