#HABARI: Polisi jijini Nairobi wanachunguza kisa ambapo Wakili maarufu katika Kaunti ya Nairobi Mathew Kyalo Mbobu, alipigwa ris…#HABARI: Polisi jijini Nairobi wanachunguza kisa ambapo Wakili maarufu katika Kaunti ya Nairobi Mathew Kyalo Mbobu, alipigwa ris…

#HABARI: Polisi jijini Nairobi wanachunguza kisa ambapo Wakili maarufu katika Kaunti ya Nairobi Mathew Kyalo Mbobu, alipigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana Jumanne jioni. Mbobu alimiminiwa risasi na kuuawa papo hapo na watu wasiojulikana waliokuwa kwenye pikipiki huku akiwa kwenye gari lake katika mtaa wa kifahari wa Karen. Maafisa wa ujasusi wameanzisha uchunguzi kubaini kiini na wahusika wa mauaji hayo ya kinyama.

Gari la marehemu alilokuwa akiendelesha lilisimama kwenye msongamano wa magari kabla ya watu waliokuwa kwenye pikipiki kumvizia na kumuua papo hapo. Mauji hayo yametikisha tasnia ya uanasheria huku mawakili na Chama cha Wanasheria cha Kenya, wakiitisha uchunguzi wa haraka katika mauaji ya wakili huyo tajika wa tajiriba ya zaidi ya miaka 29.

Mauaji hayo ya kinyama yakitokea kilomita chache na eneo alikouwawa Mbunge wa Kasipul Charles Were na watu waliokuwa kwenye pikipiki miezi minne iliyopita katika mzunguko wa City Mortuary.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania #uchaguzimkuu2025

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *