
Iran imekubali mfumo mpya wa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti usambazaji wa silaha za nyuklia IAEA siku ya Jumanne, baada ya kusimamisha ushirikiano kufuatia vita na Israel mwezi Juni.
Makubaliano hayo yalitiwa saini mjini Cairo nchini Misri na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi na Mkuu wa Shirika la IAEA Rafael Grossi, ambaye alisifu kuwa ni “hatua muhimu katika mwelekeo sahihi”.
Ulikuwa ni mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu wa Iran na IAEA tangu isitishe ushirikiano na wakala huo kufuatia vita vya siku 12 na Israel, ambapo Israel na Marekani zilishambulia vinu vya nyuklia vya Iran.
Wakiwa mjini Cairo, waziri Araghchi na Grossi walikutana na rais wa Misri Abdelfattah al-Sisi ambaye aliyasifu makubaliano hayo kama “hatua chanya kuelekea kudhibiti nyuklia.