Kongo yataka dunia itambue mauaji ya halaiki masharikiKongo yataka dunia itambue mauaji ya halaiki mashariki

Zaidi ya miongo mitatu imeisha huku eneo la mashariki ya Congo lonalopakana na Rwanda na lenye utajiri wa raslimali ya madini likikumbwa na mapigano mabaya kuwahi kutokea tangu kumalizika vita vya pili vya dunia. 

Kwa muda sasa Congo imekuwa ikiyataja mauaji yanayoendelea kwenye eneo la mashariki lenye utajiri wa madini kama mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa mashariki.

Wakati mauaji haya yamedumu sasa kwa zaidi ya miongi mitatu huku yakivuta hisia za mataifa makubwa katika miaka ya hivi karibuni hasa baada ya uasi mpya wa kundi la M23 linalodaiwa kusaidiwa na Rwanda, idadi ya watu waliouawa imepanda maradufu huku ikisababisha athari kubwa katika ukanda ambao tayari ulikabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu.

Waziri anayehusika na haki za binadamu nchini Congo Samuel Mbemba amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba wanataka kuendesha kampeini kwa ajili ya kuvunja kimya wakati ambapo hakuna mtu hata mmoja anayediriki kulitaja suala hili kama mauaji ya kimbari.

”Wananchi wanapolengwa kimakusudi kwa nia ya kuwaangamiza wote, ni vyema tuseme wazi kuwa haya ni mauaji ya kimbari.”

Tshisekedi: Ukimya kuhusu machafuko unapaswa kuvunjwa

Rwanda | DR Kongo 2025 | Gisenyi
Raia wa Kongo wanaokimbia mapigano yanayoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakiwasili katika kambi ya Rugerero huko GisenyiPicha: TONY KARUMBA/AFP

Waziri Mbemba amesema kwamba wameanzia Geneva na wanatarajia kwenda hadi New York ili kuwafanya viongozi wa dunia kulitambua tatizo la mauaji linaloendelea nchini mwao kuwa linapaswa kupewa jina linalostahili.

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la AFP Rwanda haikuweza kupatikana kutoa kauli katika madai haya ya Congo lakini akizungumza katika mkutano wa umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu, mwakilishi wa Rwanda Urujeni Bakuramutsa aliilaumu Congo kutokana na kuendesha kampeini ya kuichafua Rwanda kwa madai ambayo yanahusu utawala wake wa ndani.

Ripoti ya umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu iliyotangzwa mjini Geneva siku ya jumatano ilisema kwamba pande mbili katika mzozo wa mashariki mwa Congo zimetenda makosa makubwa yenye uhalifu wa kivita.

Akilizungumzia tatizo hilo mkuu wa ofisi ya umoja wa mataifa kuhusu hakiza binadamu Volker Turk amesema kwamba Rwanda na Congo wanawajibika kwa mujibu wa sheria za kimataifa kwa kuunga mkono makundi yenye silaha ambayo yana historia ya kutenda uhalifu.

Nani ananufaika na machafuko ya Kongo?

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Akijibu kauli hiyo waziri anayehusika na masuala ya haki za binadamu nchini Congo Samuel Mbemba amesema taarifa za Turk zimezingatia tu utafiti wake mwenyewe ambao lakini unafaa uyatamabuE mauaji hayo kama ya kimbari.

Kwa upande wake waziri wa sheria nchini Congo Guillaume Ngefa amesema kwamba jamii ya kimataifa inapaswa kusikiliza kile ambacho nchi yake inasema na kuyatambua mauaji hayo kama ya kimbari.

”Haya ni mauaji ya halaiki, haya ni machafuko ya kikabila, hii ni muhimu sana na taarifa nyingi kutoka mashirika ya kimataifa na ripoti za watafiti zilizotumwa kwa mkuu wa tume hii zinaonyesha kabisa ni mauaji yanayolenga jamii fulani.”

Amelaani makosa na visa vingine vilivyofanyika katika maeneo ya Rutshuru akivitaja kama vilivyofanywa na Rwanda na washirika wake ambapo watu zaidi ya 300 waliuawa

Hadi sasa mapigano yameendelea licha mkataba uliosainiw amwezi Juni mjini Washington katika ya serikali za Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *