Nchini Niger, mashambulizi ya kundi la Islamic State katika Sahel (ISIS) dhidi ya raia katika eneo la Tillaberi yameongezeka katika miezi ya hivi karibuni. Hii ni hitimisho la ripoti iliyochapishwa leo Jumatano, Septemba 10, na shirika la kimataifa la Human Rights Watch. Kulingana na shirika hilo, ISIS iliua watu 127 katika mashambulizi matano ilioandika, yaliyotokea kati ya mwezi Machi na Juni mwaka huu. HRW inatoa wito kwa mamlaka ya Niger kuwalinda vyema raia katika eneo hili.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo inatokana na mahojiano thelathini na mashahidi, wanaharakati, waandishi wa habari na madaktari. Kulingana na shuhuda hizi, jeshi halijajibu, licha ya maonyo yaliyotolewa.

Wapiganaji wa Islamic State katika eneo la Sahel waligharimu maisha ya makumi ya watu na nyumba kuporwa na kuchomwa moto wakati wa mashambulizi matano katika eneo la Tillaberi kati ya mwezi Machi na Juni, kulingana na ripoti ya Human Rights Watch.

Mnamo mwezi Machi, huko Fambita, washambuliaji walielekea kwenye msikiti wakati wa sala na kufyatua risasi. Shambulio kama hilo lilitokea mwezi Juni huko Manda na kuua zaidi ya watu 70. Mwezi Mei, kijiji cha Dani Fari kilishambuliwa. Wanaume watano na wavulana wawili walipigwa risasi nyingi mgongoni, kichwani, na mikononi.

Kijiji cha Ezzak kililengwa mwezi Juni. Huko Abarkaïzé, chifu wa kijiji aliuawa. Inasemekana alikataa kukusanya zakat, ushuru, kwa kundi la Islamic State katika Sahel (ISIS).

Hakuna shambulio lolote kati ya haya ambalo limedaiwa, lakini mashahidi wanayahusisha na ISIS. Mara nyingi, wanadai kuwa washambuliaji waliwashutumu kwa kushirikiana na jeshi la Niger na kwamba, licha ya onyo lao, jeshi lilishindwa kuwalinda.

Kwa hivyo Human Rights Watch inatoa wito kwa mamlaka ya Niger kuwalinda raia huko Tillaberi, kuchunguza madai haya ya uhalifu wa kivita, na kuwafungulia mashtaka wale waliohusika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *