Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen anahutubia hii leo Jumatano kuhutubia Bunge la Ulaya mjini Strasbourg, Ufaransa katika hotuba yake kuu ya kwanza ya muhula wake wa pili katika nafasi hiyo.

Katika hotuba hiyo masuala kadhaa zikiwemo mada za ushindani, usalama, ulinzi, biashara ya kimataifa na bajeti ijayo ya Umoja huo wa Ulaya yanatarajiwa kuangaziwa katika hotuba hiyo kwa wabunge. 

Bi Ursula Von der Leyen anatarajiwa kuwashawishi wabunge wa umoja huo kumuunga mkono katika miradi muhimu ya kisera kwa miaka ijayo, ikiwemo kuendelea kuiunga mkono Ukraineinayokabiliwa na vita na kuboresha uwezo wa ulinzi wa nchi za umoja wa ulaya.

Kiongozi huyo raia wa Ujerumani alichaguliwa tena kama rais wa tume hiyo na wabunge mwaka jana lakini tangu wakati huo amekuwa akikabiliwa na ukosoaji mkubwa wa kisiasa.
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *