
Rais wa zamani wa mrengo wa kulia wa Brazil Jair Bolsonaro amehukumiwa siku ya Alhamisi, Septemba 11, kifungo cha miaka 27 jela kwa jaribio la mapinduzi ya kijeshi, kwa kujaribu kuzuia kurejea madarakani kwa Rais wa sasa wa mrengo wa kushoto Luiz Inacio Lula da Silva. Hukumu hiyo itatangazwa na majaji muda mfupi baadaye.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Akiwa na umri wa miaka 70, rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 43 jela. Akishutumiwa kuwa kiongozi wa “kundi la uhalifu” ambalo lilipanga njama za kuhakikisha “kuendeleza mamlaka yake kimabavu” licha ya kushindwa kwake na Rais wa sasa wa mrengo wa kushoto, Luiz Inacio Lula da Silva, katika uchaguzi wa mwaka 2022, Jair Bolsonaro anaedelea kusema kuwa hana hatia.
Jaji Cristiano Zanin ameamua kwamba mkuu huyo wa zamani wa nchi alishiriki katika “kundi la wahalifu wenye silaha,” na hivyo majaji wanne dhidi ya mmoja kuamuwa kumhukumu kiongozi huyo wa zamani baada ya kutiwa hatiani. Jair Bolsonaro ambaye hajastahiki hadi mwaka 2030 na ambaye yuko chini ya kizuizi cha nyumbani huko Brasilia tangu mapema mwezi Agosti kwa tuhuma za kuzuia kesi yake, hajahudhuria vikao vyovyote vya kesi yake, kwa sababu za kiafya, kulingana na utetezi wake.
“Wanaita hili jaribio wakati kila mtu alijua matokeo kabla hata hayajaanza kutangazwa,” amejibu Flavio Bolsonaro kwenye mtandao wa kijamii wa X. Mtoto mkubwa wa rais huyo wa zamani amelaani “mateso ya hali ya juu.”
Mwandishi wa habari wa AFP amemwona Jair Bolsonaro siku ya Alhamisi asubuhi kwenye bustani yake, akiwa amevalia shati la kijani kibichi na suruali nyeusi, akiwa na rafiki wa karibu.
Kesi hiyo inagawanya umma ulio na mgawanyiko mkubwa, pamoja na katika mji mkuu. Jaji Moraes alikuwa wa kwanza kupiga kura siku ya Jumanne kwa ajili ya hukumu ya rais huyo wa zamani, akisema kwamba Brazil ilikuwa “karibu kuwa tena utawala wa udikteta” wakati wa madai ya kushindwa kwa mapinduzi. Jair Bolsonaro anahukumiwa pamoja na washirika saba wa karibu, wakiwemo mawaziri na majenerali kadhaa wa zamani.
Hii ni mara ya kwanza kwa mkuu wa zamani wa nchi kujibu tuhuma kama hizo, katika nchi ambayo bado inakumbukwa na kumbukumbu ya udikteta wa kijeshi (1964-1985). Flavio Dino, Waziri wa zamani wa Sheria chini ya Lula, pia alipiga kura ya kuhukumiwa kwa Bolsonaro, akibainikwamba makosa anayoshutumiwa “hayastahiki msamaha.”
Vuguvugu la kihafidhina kwa sasa linajaribu kutaka Bunge liidhinishe sheria ya msamaha kwa kiongozi wake. Tayari kwa kuzingatia rufaa zinazowezekana dhidi ya hukumu hiyo, mkuu wa zamani wa kambi ya serikali alisherehekea kura ya jaji wa tatu, Luiz Fux, siku ya Jumatano.
Hali ambayo imesababisha maandamano yaliyodumu zaidi ya saa kumi na moja, Fux hadi sasa ndiye jaji pekee aliyepiga kura kuachiliwa kwa Bw. Bolsonaro. Alifuta kesi hiyo, akashutumu ukosefu wa ushahidi, na akasema kwamba njama inayodaiwa haikuenda zaidi ya “awamu ya maandalizi.” Kura ya Jaji Fux “haitaathiri matokeo ya mwisho, lakini itaathiri historia,” mbunge wa kambi ya Bolsonaro Luiz Lima alitabiri.
Mabishano hayo yalimkasirisha Lula, ambaye ametangaza Alhamisi kwenye média local Band kuwa “Bolsonaro alijaribu kufanya mapinduzi katika nchi hii.” “Kuna dazeni, mamia ya vipande vya ushahidi,” amesema.
Mzozo kati ya Brazil na Marekani
Suala la Bolsonaro pia ni mzizi wa mzozo ambao haujawahi kutokea kati ya serikali kuu ya Amerika Kusini na Marekai. Akishutumu “madhila” dhidi ya mshirika wake wa mrengo mkali wa kulia, Rais wa Marekani Donald Trump alitoza malipo ya 50% ya adhabu kwa sehemu kubwa ya mauzo ya nje ya Brazil.
Washington pia ilibatilisha visa vya majaji kadhaa wa Mahakama ya Juu ya Brazil na kuweka vikwazo vya kifedha kwa mmoja wao, Alexandre de Moraes, ripota katika kesi ya Bolsonaro.