
Afisa wa Hamas, Fawzi Barhoum, katika hotuba aliyoitoa kwenye televisheni amesema shambulizi hilo liliulenga ujumbe wao wa majadiliano wakati ulipokuwa katika harakati ya kujadiliana kuhusiana na pendekezo la kusitisha mapigano la Rais Donald Trump wa Marekani.
Haya yanafanyika wakati ambapo Qatar kupitia waziri wake mkuu imesema Israel “imeyaua matumaini yote” ya kuachiwa kwa mateka wanaoendelea kushikiliwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza.
Matamshi hayo ya Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani yanatolewa wakati ambapo anatarajiwa kuzungumza katika Mkutano Mkuu wa Baraza la Umoja wa Mataifa leo.