
Jaji huyo Luiz Fux ametofautiana na majaji wengine wawiliwaliopiga kura ya kufunguliwa mashtaka kwa Bolsonaro na kutilia shaka uamuzi wa kesi hiyo.
Katika Mahakama ya Juu ya Brazil iliyo na majaji watano, majaji watatu wanahitajika kupiga kura ya ndiyo ili kesi isonge mbele.
Majaji wawili waliosalia bado hawajapiga kura yao. Bolsonaro anatuhumiwa kupanga njama ya mapinduzi na washirika wake dhidi ya serikali ya mrithi wake Luiz Inacio Lula da Silva, kufuatia kushindwa kwake katika uchaguzi wa mwaka 2022.
Uamuzi wa kesi hiyo unatarajiwa kutolewa Ijumaa.