Nchini Marekani, mwanaharakati maarufu wa kisiasa na mshirika wa rais Donald Trump, Charlie Kirk, ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa katika chuo kikuu cha Utah.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Trump amelaani tukio hilo na kusema ni nyakati ngumu zenye giza nchini Marekani.

Maafisa wa usalama wamewakamata washukiwa wawili, huku msako ukiendelea.

Gavana wa jimbo la Utah, Spencer Cox, ameelezea mauaji hayo kama ya kisiasa.

Baada ya mauaji hayo, chuo kikuu cha Utah kitasalia kufungwa wakati masomo yote yakiwemo ya kwenye mitandao yakisitishwa hadi Jumatatu ya wiki ijayo.

Mauaji ya mshirika huyo wa Rais Trump yamelaaniwa kutoka ndani na nje ya nchi.
Mauaji ya mshirika huyo wa Rais Trump yamelaaniwa kutoka ndani na nje ya nchi. © Caitlin O’Hara / Reuters

Katika taarifa yake, chuo hicho kimesema kimeshtushwa na mauaji hayo, wanasiasa kutoka chama cha Democratic na wale wa Republican wakilaani tukio hilo.

Viongozi wengine wa dunia akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer nao pia wamelaani mauaji hayo wakieleza kwamba machafuko ya kisiasa hayakubaliki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *