Kifo hicho kimezua hofu ya machafuko ya kisiasa nchini Marekani. Kirk aliyekuwa na umri wa miaka 31 alipigwa risasi ya shingo wakati alipokuwa akizungumza katika hafla ya chuo hicho.

Picha za video kutoka eneo la tukio zilimuonesha akihutubia umati mkubwa wa watu kabla mlio wa risasi moja haujasikika.

Kirk alionekana kuanguka kwenye kiti chake huku umati huo wa watu ukitawanyika. Idara ya Usalama wa Umma ya Utah imesema mtu aliyemshambulia alikuwa amevalia nguo nyeusi na alifyatua risasi kutoka paa la jengo lililokuwa karibu.

Mtu huyo bado hajulikani alipo, na Rais Donald Trump amewalaumu wanasiasa wa ”mrengo mkali wa kushoto” kwa mauaji hayo na ameapa kuwasaka wahusika.

Trump ameelezea tukio hilo kama “kipindi cha giza kwa Marekani.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *