Suan Kusini kuwarudisha makwao wahamiaji kutoka MarekanSuan Kusini kuwarudisha makwao wahamiaji kutoka Marekan
11 Septemba 2025

Sudan Kusini inafanya majadiliano ili kuwarejesha wahamiaji iliowapokea kutoka Marekani chini ya mpango wa Rais Donald Trump wa kuwakamata na kuwarudisha wahamiaji katika nchi walizotokea.

https://p.dw.com/p/50Lry

Polisi ya New York ikiwakamata waandamanaji wanaopinga Marekani kuwafurusha wahamiaji
Polisi ya New York ikiwakamata waandamanaji wanaopinga Marekani kuwafurusha wahamiajiPicha: David Dee Delgado/AFP

Kulingana na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Sudan Kusini,Apuk Ayuel Mayen, wizara hiyo iko katika majadiliano na nchi walikotokea wahamiaji hao ili kuwarejesha makwao.

Sudan Kusini iliwapokea wahamiaji wanane kutoka Marekani mnamo mwezi Julai.Wahamiaji hao walikuwa wamefungwa kwa makosa makubwa ya uhalifu ila ni mmoja tu miongoni mwao aliyekuwa raia wa Sudan Kusini.

Rais Donald Trump ameipa kipaumbele hatua ya kuwaondoa nchini humo wahamiaji wasio na vibali na kuwarejesha makwao au katika nchi maskini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *