Hii ni kutokana na kuhusishwa kwake na Mmarekani Jeffrey Epstein, aliyefungwa jela kutokana na madai ya kuendesha mtandao uliowadhalilisha kingono wasichana wadogo.

Katika taarifa aliyoitoa bungeni waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Stephen Doughty amesema uamuzi huo umechukuliwa kufuatia baruapepe zilizochapishwa wiki hii, ambazo Mandelson alimtumia Epstein.

“Mheshimiwa Spika baruapepe hizi zinaonesha ukubwa wa uhusiano wake na Jeffrey Epstein ni tofauti na ule uliojulikana wakati wa kuteuliwa kwake. Hasa mheshimiwa Spika, maoni yake kwamba kifungo cha kwanza alichopewa Jeffrey Epstein kilikuwa cha makosa na kinastahili kuchunguzwa, ni taarifa mpya. Na kutokana na hilo mheshimiwa Spika na kwa kuzingatia uhalifu uliofanyiwa wahanga wa Epstein kama tunavyojua sote, Mandelson ameachishwa kazi kama balozi mara moja,” alisema Doughty.

Mandelson ambaye aliteuliwa kama balozi mwezi Februari mwaka huu baada ya kile ambacho serikali ya Uingereza ilisema ni ukaguzi wa kina aliofanyiwa, ameelezea kujutia kwake kuhusishwa na Epstein na kusema alikuwa hafahamu kabisa kuhusiana na vitendo vyake vya kihalifu.

Epstein alijiuwa mnamo Agosti mwaka 2019 alipokuwa gerezani akisubiri mashtaka ya udhalilishaji wa kingono.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *