
Majai walisema rais huyo wa zamani alikula njama za kusalia madarakani licha ya kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2022.
Majaji wanne kati ya watano wa mahakama hiyo walisema kwenye hukumu hiyo ya Alhamis (Septemba 111) kwamba walimtia hatiani mwanasiasa huyo wa mrengo mkali wa kulia kwenye mashitaka matano, likiwemo la kupanga njama ya kumuua hasimu wake, rais wa sasa Lula da Silva .
Watuhumiwa wengine kwenye kesi hiyo nao pia walihukumiwa vifungo vya aina mbalimbali, akiwemo waziri wa zamani wa ulinzi, Jenerali Braga Netto, aliyehukumiwa kifungo cha miaka 26 jela.
Mawakili wa Bolsonaro , ambaye amekuwa akikanusha kutenda kosa lolote, walisema wangeliukatia rufaa uamuzi huo.
Hadi hapo, alikua bado anashikiliwa kwenye kifungo cha nyumbani mjini Brasilia.