
Msemaji wa jeshi la majini la China , Leng Guowei, ameiita safari hiyo kuwa ni ya kawaida na hailengi kumtishia yeyote.
Hata hivyo, serikali ya Taiwan imesema kuwa itachapisha muongozo mpya wa usalama kwa mara ya kwanza wiki ijayo ili kuwaelekeza raia hatua za kuchukuwa pale watakapokabiliana na “wanajeshi wowote wa maadui” ndani ya kisiwa hicho.
Taipei imesema madai yoyote ya kujisalimisha kwa kisiwa hicho kwa China yanapaswa kuchukuliwa kuwa ni uongo.
Uchapishwaji wa muongozo huo unachukuliwa kama juhudi za karibuni kabisa za Taiwan kukabiliana na shinikizo la kijeshi linaloongezeka kutoka China, ambayo inakichukulia kisiwa hicho kuwa mamlaka yake iliyoasi.