‎#HABARI: Jopo la Wataalamu na Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala wamefanikiwa kuondoa uvimbe wa kilogr…‎#HABARI: Jopo la Wataalamu na Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala wamefanikiwa kuondoa uvimbe wa kilogr…

‎#HABARI: Jopo la Wataalamu na Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala wamefanikiwa kuondoa uvimbe wa kilogramu 6.5 kwa Mwanamke mmoja mkazi wa Morogoro uliopelekea akose mtoto kwa zaidi ya miaka 10.

‎Akizungumza mara baaada ya kuondolewa uvimbe huo, Mwanamke huyo amesema baada ya kuhangaika na changamoto ya kukosa mtoto kwa zaidi ya miaka 10, takribani miezi sita iliyopita alianza kuhisi uvimbe kuongezeka ndipo aliposhauriwa kufika Hospitali ya Mwananyamala wakati alipokuwa kwa Dada yake Jijini Dar es Salaam.

‎”Kwa miaka mingi nilikuwa naishi kwa maumivu na aibu kwa sababu watu walidhani nina mimba kumbe ni uvimbe, nilipokuja Dar es Salaam kwa dada huko Kimara alinishauri nifike hapa ili kufanyiwa uchunguzi na kujua shida ni nini, hatimaye nilianza kuhudhuria na leo nafurahi kutolewa uvimbe huu kwani najihisi mwepesi” ameeleza mwanamke huyo.


‎Kwa upande wake Daktari bingwa wa Magonjwa ya wanawake na Uzazi Hospitali ya Mwananyamala Dkt. Taiba Kassim Haidar amesema mgonjwa huyo alifanyiwa vipimo vya kina baada ya kufika hospitalini miezi sita iliyopita na kubainika kuwa na uvimbe mkubwa uliokuwa unahatarisha afya yake, na kupelekea changamoto ya kukosa mtoto.

‎“Tulianza kumuona kwenye kliniki zetu alipofika na tukabaini tatizo hili linahitaji kufanyiwa upasuaji na leo tumefanikiwa kuondoa uvimbe huo wenye uzito wa kilogra 6.5 kwa mafanikio, Hali yake ni nzuri na tutaendelea kumfuatilia,” amesema Dkt. Haidar na kuongeza kuwa uvimbe huo utachunguzwa kitaalamu ili kubaini kama una hatari zaidi.

‎Jopo la wataalamu na madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, waliohusika katika zoezi hilo ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya wanawake Dkt. Taiba Kassim Haidar, Daktari wa Upasuaji Dkt. Hudhaima Issa na Dkt. Benjamini Uisso, Wauguzi Muuguzi Esther Munisi na Hafsa Ramadhani, Mtaalamu wa dawa za usingizi Pancrasi Haule, na Mteknolojia dawa Mustafa Juma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *