#HABARI: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi, amesema Madhehebu ya Dini yana Msaada mkubwa kwa Serikali katika juhudi za kudumisha Amani na Utulivu wa Taifa.
Rais Dkt Mwinyi ameyasema hayo katika Kongamno la Kuiombea Nchi Amani lililoandaliwa na Umoja wa Akinamama wa Kikristo na Maendeleo Zanzibar lililofanyika Ukumbi wa Dkt, Ali Muhammeid Shein, Tunguu,Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema Amani ni Neema kwa Maendeleo ya Wanaadamu inayopaswa kuenziwa na Kudumishwa na kila mmoja kwa Mustakabali wa Taifa Rais Dkt, Mwinyi amewasizistiiza Viongozi wa dini kuwa wana wajibu Mkubwa wa kutumia nafasi zao kuwaelimisha Waumini Umuhimu wa Amani pamoja na Kuwaandaa kuwa Raia wema.
Rais Dkt, Mwinyi, amewahakikishia akinamama hao wa Kikristo kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha inazipatia Ufumbuzi Changamoto zote zinazozikabili Taasisi za Dini ili ziweze kutekeleza Wajibu wao Ufanisi na Amani. Ameupongeza Umoja huo kwa kuandaa Kongamno hilo alillolielezea kuwa ni la umuhmu Mkubwa wakati huu Nchi ikielekea katika Uchaguzi Mkuu.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.