#HABARI: Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU Mkoa wa Ilala imefanikiwa kuokoa zaidi ya Shilingi Milioni 13 zilizotokana na vibali vya ujenzi kwenye mradi wa ujenzi wa ghorofa lililopo Mtaa wa Kongo na Rufiji Plot 89 Block M.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ilala Bw. Faustine Maijo, ghorofa hilo lilijengwa bila kuwa na vibali kutoka kwa Mamlaka husika ikiwemo Bodi ya Halmashauri ya Jiji, Bodi ya Usajili wa Wakandarasi na Bodi ya Usajili wa Wahandisi.
Pia katika kipindi cha Mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu Taasisi hiyo imefanya warsha katika Sekta za Elimu na Ardhi iliyotokana na uchambuzi wa mifumo wa usimamizi wa miradi inayotelezwa kwa fedha za wafadhili katika Jiji la Dar es Salaam na kubaini baadhi ya mapungufu katika utekelezaji na usimamizi wa miradi hiyo.
Katika hatua nyingine Taasisi hiyo imepokea taarifa za malalamiko 59, ambapo kati ya hizo taarifa 38 zilihusu rushwa na kushughulikiwa kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Ruhswa.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania #uchaguzimkuu2025