
Akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja cha televisheni siku ya Alhamis (Septemba 11), Araghchi alisema Shirika la Nishati ya Atomiki la nchi hiyo linaendelea kutathmini hali na upatikanaji wa shehena hiyo ya urani.
Kauli hiyo ilitolewa baada ya Iran na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) kukubaliana juu ya mfumo mpya wa ushirikiano siku ya Jumanne (Septemba 9).
Tehran ilikuwa imesitisha mahusiano na shirika hilo kufuatia vita vya siku 12 vya mwezi Juni, ambapo Israel na Marekani zilivipiga mabomu vinu vya nyuklia.
Iran inaituhumu IAEA kwa kushindwa kuyalaani mashambulizi hayo.