Hata hivyo, waziri mkuu huyo ambaye pia ndiye waziri wa mambo ya kigeni wa taifa hilo la Kiarabu, alithibitisha kwamba nchi yake isingelizilekeza juhudi za kukomesha vita vinavyokaribia miaka miwili sasa kwenye Ukanda huo.

Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani alikiambia kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamis (Septemba 11) kwamba Israel ilikuwa imechupa mipaka na miiko yote ya kimataifa kwa mashambulizi yake katika mji mkuu wa Qatar wiki hii, ambayo yaliingilia mamlaka ya taifa hilo la Ghuba na kutishia usalama wa eneo zima.

Mashambulizi hayo ya siku ya Jumanne (Septemba 9) yaliwauwa watu sita, wakati viongozi wa Hamas wakiwa wamekusanyika kujadili pendekezo la usitishaji vita vya Gaza lililotolewa na Marekani .

Mashambulizi hayo yanahofiwa kutatiza mchakato wa amani unaosimamiwa na Misri, Qatar na Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *