#HABARI: Kijana wa miaka 22 kutoka Utah amekamatwa kwa mauaji ya mwanaharakati wa mrengo wa kulia Charlie Kirk, ambaye alipigwa risasi akiwa jukwaani kwenye hafla ya chuo kikuu mapema wiki hii huko nchini Marekani.
Tyler Robinson aliwekwa kizuizini siku ya Alhamisi usiku, baada ya msako wa saa 33 ambao ulikamilika baba yake aliposaidia kumshawishi ajisalimishe kwa Polisi.
Kukamatwa kwake kulitangazwa kwa mara ya kwanza na Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alimtaka mshukiwa huyo kukabiliwa na hukumu ya kifo.
Mauaji ya Kirk, ambaye alipigwa risasi alipokuwa akijadiliana na wanafunzi siku ya Jumatano, yamewashtua Wamarekani na kuweka wazi migawanyiko mikali juu ya vyama nchini humo.
Wachunguzi walisema katika kikao na wanahabari siku ya Ijumaa kwamba mshukiwa alikiri kwa baba yake na kusema afadhali ajiue badala ya kujisalimisha. Kisha baba huyo alimwita mchungaji kijana ambaye ni rafiki wa familia.
Wote wawili walijaribu kumtuliza mshukiwa, polisi walisema. Mchungaji huyo, ambaye pia anahudumu kama afisa wa usalama wa mahakama, baadaye aliwapigia simu wanajeshi wa Marekani, ambao walimshika mshukiwa mwendo wa saa 22:00 kwa saa za eneo siku ya Alhamisi.
Gavana wa Utah Spencer Cox alisema kuwa picha za uchunguzi zilionyesha Bw Robinson akiwasili katika chuo kikuu cha Utah Valley takriban saa nne kabla ya tukio la mlio wa risasi kushuhudiwa, na kumuua Kirk huku wanafunzi kukikimbia kujificha.
Cox aliwaambia waandishi wa habari kwamba wakati Bw Robinson aliwekwa kizuizini, alikuwa amevalia mavazi sawa na yale yaliyoonekana kwenye kamera za CCTV katika eneo la ufyatuaji risasi.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania #uchaguzimkuu2025