Rais wa Iran Massoud Pezeshkian siku ya Jumatatu, Septemba 15, ametoa wito kwa nchi za Kiislamu kuvunja uhusiano na Israel kabla ya mkutano wa kilele uliopangwa kufanyika mjini Doha ili kujibu shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa lililotekelezwa wiki iliyopita na Israel dhidi ya Qatar kuwalenga maafisa wa Hamas, shirika la habari la AFP limeripoti.
