Nchini Guinea, kampeni ya kura ya maoni ya katiba inaingia katika hatua yake ya mwisho kabla ya upigaji kura siku ya Jumapili, Septemba 21. Kipindi hiki kinaingiliana na kusimamishwa kwa vyama vikuu vya kisiasa, UFDG cha Cellou Dalein Diallo na RPG chaa Alpha Condé, ambavyo vinatoa wito wa kususia uchaguzi. Ni utawala wa kijeshi na serikali pekee ndio wanaandaa mikutano ya kura ya “ndio”. Miongoni mwa mambo yenye utata zaidi ya Katiba: kuundwa kwa Bunge la Seneti.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Conakry, Tangi Bihan

Idhini ya Mamadi Doumbouya kugombea katika uchaguzi wa urais, wakati katiba ya mpito ilimkataza kufanya hivyo, si hoja pekee ya rasimu ya Katiba mpya ambayo inazua utata. Swali kuhusu taasisi pia linagawanya raia: je ni muhimu kuunda Bunge la Seneti, pamoja na Baraza la Wawakilishi?

Katika soko kubwa la Madina, ambalo halikuwa na shughuli nyingi siku ya Jumapili, Septemba 14, Saikou alikuja kununua nguo. Anafuatilia kwa karibu kampeni ya kura ya maoni. Kwake, kuunda Bunge la Seneti ni wazo zuri: “Itaboresha uwakilishi wa watu katika utofauti wao na kuleta taasisi karibu na raia. Kwa Bunge pekee, viongozi waliochaguliwa wako mbali sana na wananchi. Pamoja na Bunge la Seneti, viongozi waliochaguliwa wataweza kuwa karibu na raia; kutahimiza ushiriki wa raia katika maisha ya kisiasa.”

Rais kuwa na mamlaka mengi makubwa

Iwapo rasimu ya Katiba itapitishwa, theluthi mbili ya maseneta watachaguliwa na madiwani wa mikoa na manispaa. Theluthi moja itateuliwa moja kwa moja na Rais wa Jamhuri. Kifungu kilichokosolewa na Ousmane, muuzaji wa bidhaa za usafi: “Si sawa kwa rais kuwa na mamlaka ya kuteua maseneta; itampa mamlaka makubwa. Mbali na hilo, sidhani kama ni muhimu kuunda Bunge la Seneti; Bunge linatosha. Sisi Waguinea ni maskini.” Ni lazima tuizuie Serikali kufanya matumizi yasiyo ya lazima. Badala yake inapaswa kuweka akiba.”

Kampeni inakamilika siku ya Jumatano jioni, Septemba 17, kabla ya siku tatu za kutafakari jinsi uchaguzi utafanyika. Wakati huo huo, zoei la usambazaji wa kadi za wapigakura linaendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *