Mkataba huo unakataza ruzuku kwa ajili ya meli zinazochangia uvuvi haramu, usioripotiwa na usiodhibitiwa lakini pia uvuvi kwenye bahari kuu.
Utafiti wa mwaka 2019 uliochapishwa kwenye jarida la Marine Policy uligundua kuwa ruzuku za uvuvi zilifikia dola bilioni 35 kwa mwaka, dola bilioni 22 kati ya hizo zikitumika kwa ajili ya kuongeza uwezo wa uvuvi.
Hata hivyo kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) asilimia 35.5 ya zaidi ya samaki 2,500 waliofanyiwa tathmini duniani kote walikuwa chini ya uvuvi huo wa kupindukia.
WTO: Makubaliano yanazingatia mazingira endelevu
China, Umoja wa Ulaya, Marekani, Korea Kusini na Japan zilitajwa katika ripoti hiyo ya Sera ya Bahari kama watoaji wakubwa zaidi wa ruzuku.
Na wakati Marekani, Ulaya, China na Brazil wakiwa miongoni mwa nchi walizochukua hatua, India na Indonesia – ambayo yana viwango vya juu vya uvuvi bado hazijasaini makubaliano hayo ya mwaka 2022.
Mkurugenzi Mkuu wa WTO Ngozi Okonjo-Iweala amesema makubaliano hayo, ambayo ni ya kwanza ya shirika hilo yanayozingatia mazingira uendelevu, “hulinda riziki za mamilioni ya watu.”
“Mafanikio haya sio tu kwa sayari na bahari lakini pia kwa wanadamu kila mahali, haswa vizazi vichanga,” alisema.
Shirika la uhifadhi wa mazingira na viumbe hai WWF pia liliyakaribisha makubaliano hayo. Anna Holl wa shirika hilo amesema “Bahari zimeunganishwa duniani kote; samaki hawajui mipaka. Ikiwa tunataka kuendelea kula samaki ni lazima hifadhi ilindwe duniani kote na makubaliano ya kimataifa ambayo kila mmoja anayazingatia.”
Kundi hilo la wanamazingira pia linaisisitizia jumuiya ya kimataifa kutopoteza mwelekeo wa hatua zinazofuata, zikiwemo utekelezaji na makubaliano zaidi ya kuziba mapengo yaliyosalia, ikiwa ni pamoja na kusitisha ruzuku zinazochangia kuzidisha uwezo wa meli.